Change Language

Ad Unit (Iklan) BIG

Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao

Post a Comment

 



🚨 OFFICIAL & CONFIRMED:

Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao kutoka Asec kwa Mkataba wa mwaka mmoja.

Yao (26) 🇮🇪 anahesabika kuwa beki bora wa kulia pia na ubora wa kucheza kama winga mshambuliaji na kupiga krosi  za mabao.

MFAHAMU KOUASSI ATTOHOULA.

Jina kamili: KOUASSI ATTOHOULA YAO.

Watu wa nyumbani kwao wanapenda kumuita kwa jina la KOUASSI ATTOHOULA YAO.

Raia wa Ivory coast

....Alizaliwa Anyama,Ivory coast

mnamo Dec 20,1996 (Age 26)

Ana urefu wa 1.68m.

Wakala :VV Consulting.


⬛ Nafasi anayochezea ni beki wa kulia

.... Nafasi nyingine anayoweza kucheza ni beki wa kushoto/winga.


Alianza maisha ya soka kwenye akademi ya Mimosas na kuitumikia akademi hiyo kwenye vikosi vya U17 na U19.


✅Julai  1,2017 akasajiliwa na klabu ya  Williamsville ya nchini humo akitumikia kwa miaka miwili.

✅Akauzwa kwenda klabu ya O.Khouribga ya nchini Morocco Jan 16,2019 aliitumikia kwa miezi 6 kisha akatolewa kwa mkopo kwenda kwenye klabu ya  Kawkab Marrak mnamo Julai 17,2019.


✅ Mnamo Sep 15,2019 baada ya mkataba wa mkopo kuisha  alirejea kwenye klabu yake ya O.Khouribga.

Na mkataba wake ndani ya klabu hiyo uliisha miezi miwili baade.


✅🟡Ndipo akajiunga tena na klabu ya Asec Mimosas ya Wakubwa Nov 9,2020.


 MASHINDANO YA CAF KAMA MCHEZAJI

✅ Amecheza jumla ya mechi 35 ya mashindano haya ya CAF ngazi ya vilabu.

...CAFCL

Amecheza mechi 27, kati ya hizo ni mechi 5 tu alitokea benchi.

..... CAFCC

Amecheza mechi 8, kati ya hizo ni mechi 1 tu alitokea benchi.


Akiwa ligi ya Morocco alicheza mechi 9 na kufunga goli 1.


Aug 27 mwaka jana akiwa na umri wa miaka 25,miezi 8 na siku 7 alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast chini ya kocha Jean Louis Gasset.

Mpaka sasa ameichezea hiyo ya taifa (michuano ya CHAN,na timu ya taifa ya pamoja) michezo 6.


Aliwahi kuwa beki bora wa msimu wa ligi kuu Ivory Coast 2021/22.

 Alikuwa miongoni kwa walioiunda kikosi bora cha msimu ligi kuu ya Ivory Coast kwenye msimu wa 2021/22 na msimu uliopita wa 2022/23


 Mshindi wa Makombe mawili ya Ligi kuu Ivory Coast

 Mshindi wa  Makombe mawili ya FA.


Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter