Change Language

Ad Unit (Iklan) BIG

MMOJA AONDOKA YANGA, WAKILI SIMON PATRICK AKABIDHIWA MIKOBA



TAARIFA: Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga imefanya Kikao Chake cha Kwanza cha Kikatiba leo Jumamosi Tarehe 30 Julai 2022, Serena Hotel jijini Dar es salaam chini ya Uenyekiti wa Rais wa Klabu Eng. Hersi Ally Said.


Pamoja na mambo mengi yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho Kamati ya Utendaji ilipokea na kujadili pendekezo la Bw. Senzo Hammilton Mazingiza la kutokuongeza mkataba wake unaoisha tarehe 31 Julai 2022.


Bw. Senzo aliwasilisha ombi hilo lenye mkutadha wa sababu za kifamilia ambayo amekuwa nayo mbali kwa kipindi cha takribani miaka mitatu.


Ombi hilo lilipokelewa na baada ya kujadiliwa, Kamati ya Utendaji ilikubali ombi hilo na kumteua Wakili Simon Patrick kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa mpito (Interim Chief Executive Officer).


Aidha, Klabu ya Yanga inamshukuru Bw. Senzo kwa utumishi wake ulio bora hasa katika mchango wake kwenye eneo la utawala na kumtakia kila la heri.


KWA UFUPI



SENZO KUONDOKA YANGA, WAKILI SIMON PATRICK AKABIDHIWA MIKOBA


Klabu ya Yanga imetangaza kutomuongezea Mkataba Afisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza anayemaliza mkataba wake kesho Julai 31, 2022 


Yanga imesema Senzo ndiye ameomba kutoongezewa mkataba kutokana na sababu za kifamilia. Wakili Simon Patrick ameteuliwa kukaimu nafasi


Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter