Change Language

Ad Unit (Iklan) BIG

Siri Ya Yanga na Bruno Ngomezi Yavuja

Post a Comment

 


BRUNO Gomez, ni mingoni mwa wachezaji ambao wapenzi wa Yanga  walitamani kumuona kikosini mwao  msimu huu, chanzo changu ndani ya Singida  FG, kimefunguka kuwa pamoja na watu wa Yanga kumtamani Bruno,  lakini Mbrazil huyo hakubaliki na uongozi wa juu pamoja na makocha wao.


“Kuna viongozi wa juu kabisa Yanga hawamkubali Bruno. Wanasema bado anahitaji muda zaidi wa kukomaa  kumudu kucheza Yanga japo wanaukubali uwezo wake. Nadhani  hata makocha (wa Yanga), hawamkubali sana ndio maana hukuona nguvu ikiwekwa kumsajili,” 


Kocha wa Singida, Hans van der Pluijm  alipoulizwa iwapo kiungo huyo ana  nafasi katika kikosi cha Yanga, alisema:  “Bruno ni mchezaji mzuri, ila bado anahitaji kukua zaidi kuweza kuhimili kucheza Yanga. Kuchezea Yanga au  Simba si kitu kidogo, kule unahitaji uwe  umekomaa hasa kuweza kukabiliana na presha za mchezo na mashabiki. “Kule  Yanga anaweza kukosea mara moja,  mara mbili, mara tatu... mashabiki  wakamzomea na kumtoa kabisa  mchezoni, hivyo anatakiwa kubaki hapa  (Singida) ili aendelee kukomaa zaidi.

SOMA ZAIDI...

.

.

.

Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter